• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua-pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Kata
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio

Hospitali Tembezi yatibu 644, Waziri Jaffo azindua rasmi

Imewekwa tarehe: June 27th, 2018

HUDUMA za matatibu kwa mfumo wa Hospitali Tembezi iliyoanza Jumatatu Juni 25, 2018 inaendelea katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Dodoma Mtakatifu Gemma iliyopo Kata ya Miyuji Jijini humo ambapo mpaka sasa jumla ya wagonjwa 664 wamehudumiwa ndani ya siku mbili za Jumatatu na jumanne.


 Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ernest Njile, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali wamekutana pamoja kutoa huduma za kiwango cha hali juu ambapo kati ya wagonjwa 664 waliohudumiwa, wagonjwa 26 wamefanyiwa upasuaji wa mifupa na wa kawaida na zaidi ya wagonjwa 38 wanatarajiwa kupasuliwa leo Jumatano Juni 27.


 Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo Hospitalini hapo leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jaffo aliipongeza Halmashauri ya Jiji na wadau wote kwa kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa Afya za Watanzania na kwamba huduma wanayoitoa ni ya kujitoa na ni ibada kubwa mbele ya Mungu.

 Alisema kuwa, amepita katika wodi mbalimbali na kushuhudia wagonjwa wanavyopatiwa huduma ambapo baadhi yao walikuwa wamekata tamaa ya kupata matibabu lakini wamepata matumaini mapya baada ya kusogezewa huduma hiyo ya kibingwa.


Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi alitoa wito kwa wananchi hususan wakazi wa Jiji kujitokeza kupata huduma hiyo iliyosogezwa karibu zaidi, ikiwa ni juhudi za Serikali za kuwafikishia Wananchi wake huduma.

 Naye Mstahiki Meya wa Jiji hilo Profesa Davis Mwamfupe awataka madiwani wenzake kuhamasisha Wananchi katika Kata zao ili wajitokeze kwa wingi kupatiwa huduma za Afya na wataalam hao waliobobea.


 Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana na Ajira ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde aliiomba Serikali kupitia kwa Waziri Jaffo kulipatia Jiji la Dodoma fedha za ujenzi wa kituo cha Afya katika Kata ya Miyuji ili kisaidie kuhudumia wagonjwa wengi wanaotegemea Hospitali Teule ya Wilaya Mtakatifu Gemma.


Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Hamadi Nyembea alisema huduma hiyo inafanikishwa na Jiji kwa kushirikiana na Hospitali mbalimbali ikiwemo Benjamini Mkapa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, na inatarajiwa kuendelea hadi Ijumaa Juni 29, 2018.

Matangazo

  • Tangazo: Maombi ya Leseni ya Vileo January 22, 2019
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2018 haya hapa: January 24, 2019
  • Mafunzo ya Utengenezaji wa Bidhaa za Ngozi (Viatu, Mipira na Mabegi) August 17, 2018
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Manispaa ya Dodoma March 27, 2018
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Prof. Mwamfupe:Wanaonyanyasa Wanawake, Watoto 'kusakwa'

    February 20, 2019
  • Madarasa 44 yaandaliwa kidato cha kwanza

    February 16, 2019
  • Austria yaalikwa kuwekeza kwenye Zabibu

    February 15, 2019
  • Jiji laahidi sare Wanafunzi mahitaji maalum

    February 14, 2019
  • Angalia zote

Video

Uzinduzi wa tovuti mpya za mikoa na halmashauri nchini
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge
  • Baraza la Mitihani

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    CDA Street

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe za Watumishi: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

Idadi ya watembeleaji

Ghostwriter

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.